August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge lamaliza mzizi wa fitina Colombia

Juan Manuel Santos, Rais wa Colombia (kushoto) akitoa mkono kwa kiongozi wa waasi wa FARC, Rodrigo Londono 'Timoshenko'

Spread the love

BUNGE la Colombia la ridhia makubaliano ya amani kati ya serikali ya nchi hiyo na kundi la waasi la FARC kufuatia vita vilivyo dumu kwa miaka 50 sasa, anaandika Wolfram Mwalongo.

Uamzi huo wa Bunge umefuatia marekebisho ya mkataba uliosusiwa awali na wananchi wa taifa hilo waliopinga kuwaruhusu waasi kushiriki shughuli za siasa katika taifa hilo jambo ambalo lilizua sintofahamu kwa wakolombia hususan waliochoshwa na vita.

Ambapo kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo mkataba huo ulipaswa kupelekwa kwa wananchi ili kupigiwa kura ya maoni lakini wakolombia kwa sauti moja walikubaliana upitishwe na Bunge la maseneta kwa niaba yao.

Katika kuunga mkono jitihada za Rais wao Juan Manuel Santos ambaye Oktoba 8 mwaka huu alipokea tuzo ya amani ya Nobel kutokana na mchango wake mkubwa wa kurejesha amani kwa taifa lake, hatimaye azma yake imetimia.

Rais huyo amekuwa akifanya majadiliano na Rodrigo Londono Kiongozi waasi hao maarufu kwa jina la ‘Timoshenko’ huko Havana nchini Cuba ambako harakati hizo zilianza mwaka 2011

Mbali na mafanikio yaliyofikiwa na taifa hilo Rais Santos alionesha wazi kufarijika na namana alivyo pata uungwaji mkono kutoka kwa Timoshenko huku shauku kubwa ilikuwa ni kukamilisha zoezi hilo katika kipindi kifupi ingawa haijawa hivyo.

“Haitakuwa kazi rahisi kwa sababu bado kuna mambo magumu tunayopaswa kukubaliana, lakini hayo ndio maelekezo tuliyoyatoa kwa ujumbe wetu, wanapaswa wakamilishe mkataba haraka iwezekanavyo,” alisema rais Santos.

Hivi sasa waasi walioko porini wanapaswa kurejea katika kambi maalumu zilizotengwa kwa ajili ya kuwahifadhi wakati shughuli za kuandaa makazi ya kudumu zikiendelea. Hata hivyo bado kumekuwa na minong’ono miongoni mwa wananchi wa taifa hilo wanao dai kulipwa fidia kufuatia vifo vya wapendwa wao waliofariki wakati wa mapigano na waasi wa FARC.

error: Content is protected !!