July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge la Katiba, wizi mtupu

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwa katika moja ya vikao vyake

Spread the love

BUNGE Maalum la Katiba, halikufikisha theluthi mbili ya kura zilizohitajika na sheria kupitisha Katiba Mpya, MwanaHALISI Online limeelezwa.

Taarifa kutoka ndani ya Bunge Maalum na serikali zinasema, bunge hilo halikupata theluthi mbili ya kura, kama ambavyo mwenyekiti wake, Samwel Sitta anavyotaka kuaminisha umma.

Mtoa taarifa wa gazeti hili ambaye alishiriki vikao vya mkakati amesema, “Theluthi mbili haikupatikana; bali theluthi mbili inayotajwa, imepatikana kwa udanganyifu.”

“Hapa hakukuwa na theluthi mbili. Kilichopo ni udanganyifu na wizi wa kura,” ameeleza mtoa taarifa huyo ambaye ni ofisa Bunge Maalum.

Taarifa zinasema, kazi ya kuchakachua kura ilifanywa kwa ustadi mkubwa usiku wa manane wa kuamkia Alhamisi 2 Oktoba 2014. Walioshiriki vitendo hivyo, ni baadhi ya maofisa usalama ambao walielekezwa na Sitta.

“Kazi hii imefanywa na mkuu wa idara ya siasa ya usalama wa taifa George Mwagha, afisa usalama wa mkoa wa Dodoma, Mama Amos pamoja na maafisa wengine wa usalama kadhaa. Walifanya kazi hii kwa pamoja na Said Yakub Othman, mfanyakazi wa Bunge chini ya maelekezo ya Sitta,” ameeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.

Amesema, “Wao ndio waliofanya kazi ya kughushi na kubadili kura zilizokataa katiba. Kazi hii ilimalizika majira ya saa tisa usiku.”

Habari zinasema, baada ya mradi wa wizi kura kukamilika, kumepangwa mkakati wenye lengo la kusambaratisha Muungano wa Kutetea Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Mkakati juu ya UKAWA umelenga kusambaza propaganda kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kwa lengo la kuaminisha wananchi kuwa baadhi ya wajumbe wa umoja huo walipiga kura kuunga mkono rasimu.

Muungano wa UKAWA uliondoka bungeni katikati ya mjadala kwa kile walichoita, “Rasimu inayojadiliwa imetupa maoni ya wananchi.” Wakatuhumu viongozi wa Bunge Maalum kuendesha ubaguzi bungeni na viongozi wakuu wa serikali kufanya vitendo vya Intarahamwe.

Propaganda kwamba baadhi ya wajumbe wa UKAWA wamepiga kura, tayari imeanza kuenezwa na Sitta. Tayari mwanasiasa huyo aliyeapa kupitisha rasimu yake kwa gharama yoyote ile, amewataja wajumbe wawili wa Chadema, Mariam Msabaha na Mwanamrisho kuwa walipiga kura.

Hata hivyo, Msabaha na Mwanamrisho, tayari wamekana kushiriki zoezi la upigaji kura.

Wamekiri kushawishiwa mara kadhaa na Sitta ili wasaliti Chadema; lakini wamesisitiza, “Hatujapiga kura. Wawatafute wengine wawasingizie.”

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, Sitta alituma mfanyakazi mmoja wa Bunge, Suleiman Haji Suleiman katika nchi za India na Saudia, ili kupigisha kura baadhi ya wajumbe.

Miongoni mwa wajumbe waliotumiwa kura nje ya nchi, ni pamoja na Mohammed Raza; Mauwa Daftari; Asha Dodo Mtwangi; Salim Hassan Turky; Amina Andrew na Shawana Bukhet.

Sulemain alipigisha kura hizo na kisha akazituma kwa njia ya mtandao kupitia simu yake ya Smartphone ya kichina yenye modem ya Huawei.

Mmoja wa wajumbe hao, alipiga kura ya hapana katika ibara zote za katiba, lakini Sitta ameutangazia ulimwengu kuwa hakuna kura iliyokataa.

“Vijana walinasa na kuzuia kura hizo kwa muda zisifike Dodoma. Walikuwa na uwezo wa kuzibadili kwa kuweka kura tofauti na walivyopiga wahusika. Nakuambia hivi, zoezi zima limetawaliwa na udanganyifu,” ameeleza mtoa taarifa.

error: Content is protected !!