August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge la Congress kufanya maamuzi kwa Trump

Spread the love

BUNGE la Congress limetaka Urusi iadhibiwe kwa kosa la kuingilia uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka jana nchini Marekani, anaandika Catherine Kayombo.

Bunge hilo linatarajia kupiga kura kesho ili kupitisha mswaada huo wa sheria unaopanga kuitaka ofisi ya rais wa Marekani kutoingilia hatua za kidiplomasia zitakazochukuliwa dhidi ya Moscow, mji mkuu wa Urusi.

Kupitishwa kwa sheria hiyo na Bunge la Congress kutamnyima Trump uwezo wa kuondoa kikwazo chochote kitakachopitishwa dhidi ya Urusi.

Aidha, Trump ameunga mkono makubaliano hayo yasiyopendelea upande wowote licha ya kwamba White House ilipinga mswaada huo hapo awali.

Kukataa kupitisha mswaada huo kungeonyesha ushirikiano wa Trump na Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Mswaada huo pia unaruhusu vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, Iran pamoja na Syria. Urusi imeendelea kukataa shutuma za kujihusisha na uchaguzi nchini Marekani na kusisitiza kutokuwa na mamlaka ya kuingilia maamuzi ya kidiplomasia.

error: Content is protected !!