Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge kutotumia neno chama tawala, upinzani 
Habari za SiasaTangulizi

Bunge kutotumia neno chama tawala, upinzani 

Bunge la Tanzania
Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri amesema, chombo hicho cha kutunga sheria, kipo kwenye mjadala mzito wa kutafuta majina ya utambulisho kwa wabunge wa chama tawala na upinzani. Anaripoti Danson Tibason, Dodoma … (endelea).

Amesema, jina linayotumika kwa wabunge wa upinzani ‘mpinzani’, halileti maana na kwamba linasababisha kudhani kuitwa mpinzani, ni kupinga kila kila kitu.

Pia amesema, wabunge wa chama tawala wanadhani, kuitwa hivyo ni kukubali kila jambo, akisema dhana hizo haziko sawa.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Novemba 2019, wakati akifunga Bunge la Sita la Bunge la Vijana kutoka vyuo vikuu nchini, lililofadhiliwa na Taasisi ya Mpango wa Maendeleo Duniani (UNDP), kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.

“Kimsingi kwa sasa Bunge tupo kwenye mjadala mzito sana wa kutafuta namna ya kupata majina mazuri ya kutumia ndani ya ukumbi  wa Bunge na nje ya bunge, mfano; tumekuwa tukisema wabunge wa upinzani, wanatoka katika vyama vya upinzani.

“Lakini majina hayo siyo mazuri, ukishasema mbunge wa upinzani na anatokea chama cha upinzani, mbunge huyo anafikiria kila kitu ni kupinga tu. Au ukishasema kuwa ni mbunge wa chama tawala, anafikiria kila kitu ni kukubali tu, nadhani jambo hili siyo zuri,” amesema Spika Ndugai.

Amesema, Tanzania haitakuwa ya kwanza kufikiri na hata kufikia uamuzi huo kwa kuwa, yapo mabunge ambayo yameepuka maneno hayo (wapinzani, tawala).

“Mnajua hata wenzetu ambao ni Umoja wa Jumuiya ya Madola, wanatumia majina tofauti na sisi. Wao wanajitambulisha kwa kusema mimi ni mbunge ninayetokea chama cha wabunge wachache na mwingine anajitambulisha kama mwakilishi  kutoka katika chama chenye wabunge wengi, na kinachofuatia ni kubishana kwa hoja,” amesema.

Spika Ndugai amefafanua, kwamba baadhi ya wabunge wa upinzani wakati mwingine wanatengewa bajeti kubwa kwenye majimbo yao, lakini hujikuta wakigomea bajeti kutokana na msimami wa chama ‘upinzani.’

“Unaweza kuona Bunge linapitisha bajeti ambapo ndani ya hiyo bajeti, kuna mishahara ya wabunge, walimu, afya pamoja na mambo mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Lakini kutokana na kuwa chama hicho ni cha upinzani, wabunge wake wanaikataa hiyo bajeti. Unaweza kukuta mbunge wa upinzani ametengewa bajeti kubwa kuliko mbunge wa  chama tawala, lakini kutokana na misimamo ya chama husika, anakataa,” amesema.

Na kwamba, mbunge wa chama tawala hudhani kila kitu ni kukubali “unaweza kusikia kuwa Bunge tunataka kufuta jimbo la Kongwa, kwa kuwa umezoea kukubali, unasema ndiyooo! Baadaye ukiulizwa, unashangaa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

error: Content is protected !!