August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge: Kumradhi Mbowe

Spread the love

MUSSA Zungu, Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana amemtaka radhi Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, anaandika Faki Sosi.

Zungu amemwomba radhi Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai kwa kushindwa kumtaja kwenye orodha ya watu waliotoa misaada kwa waathirika wa Tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani Kagera siku chache zilizopita.

“Nakubali sikumtaja. Nimombe radhi kwa sababu yeye amehusika. Suala hili halipaswi kutugawa,” amesema Zungu ambaye ni Mbunge wa Ilala (CCM).

Mikoa ya Kanda ya Ziwa ilikumbwa na tetemeko la ardhi tarehe 11 Septemba mwaka huu na kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na vifo 17, nyumba na shule kubomokapia kuacha majeraha kwa wakazi wa maeneo hao.

Zungu ameomba radhi baada ya Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga (Chadema) kuomba mwongozo na kutaka kujua sababu za mwenyekiti huyo kutomtaja Mbowe ambaye ni miongoni mwa viongozi waliofika Kagera na kutoa misaada katika siku za mwanzo za tukio.

Kwenye kauli yake, Waitara alisema wakiwa wabunge wa upinzani, walichanga Sh. 1,000,000 kila mmoja kwa ajili ya kuzipeleka Kagera kutokana na kuwepo kwa madhara ya tetemeko hilo.

Katika eneo la tukio Mbowe ameongozana na viongozi wengine wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akiwemo James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi.

 

error: Content is protected !!