August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge kujadili miswada 9

Spread the love

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaanza leo mjini Dodoma huku likitarajia kujadili miswada sita na kuipitisha, anaandika Dany Tibason.

Owen Mwandumbya, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu shughuli zitakazofanyika katika Bunge hilo.

Aliitaja miswada itakayojailiwa na kupitishwa kuwa ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa Mwaka 2016, Muswada wa Sheria ya Udhamini na Usajili wa Wadhamini wa Mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016.

Miswada mingine ni Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Taaluma ya Mkemia wa Taaluma ya Kemia wa Mwaka 2016, Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Kilimo wa Mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Uvuvi wa Mwaka   2016.

Mwandumbya amesema, katika mkutano huo wa Bunge maswali yasiyopungua 110 na maswali kwa Waziri Mkuu yasiyopungua 10 yataulizwa.

Kwa mujibu wa Mwandimbya, Bunge linatarajiwa kuhitimishwa na kuahirishwa Septemba 16 mwaka huu.

error: Content is protected !!