Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge kuhitimishwa Juni 16, Bajeti kujadiliwa siku mbili
Habari za Siasa

Bunge kuhitimishwa Juni 16, Bajeti kujadiliwa siku mbili

Bunge la Tanzania
Spread the love

BUNGE la 11 la Tanzania linaloongozwa na Spika Job Ndugai, litahitimishwa Jumanne ijayo tarehe 16 Juni 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ratiba iliyotolewa leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020 na Ofisi ya Bunge la Tanzania inaonyesha, Rais wa Tanzania, John Magufuli, atahutubia Bunge hilo Jumanne ijayo saa 3 asubuhi.

Awali, ratiba ilikuwa ikionyesha Bunge hilo ambalo Rais Magufuli alilizindua tarehe 20 Novemba 2015, lingehitimishwa tarehe 19 Juni 2020.

Katika ratiba hiyo mpya, kesho Alhamisi tarehe 11 Juni 2020 itawasilishwa taarifa ya hali ya uchumi na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/2021.

Ijumaa na Jumamosi tarehe 12 na 13 Juni 2020 itakuwa ni mjadala kuhusu taarifa ya hali ya uchumi na bajeti ya serikali huku Jumatatu ya tarehe 15 Juni 2020 itahitimishwa.

Mjadala wa bajeti hiyo itajadiliwa kwa siku mbili ikiwa ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo bajeti ilikuwa ikijadiliwa kwa siku saba.

Jumatatu hiyo hiyo ya tarehe 15 Juni 2020, Bunge litapiga kura ya Bajeti ya Serikali, Kujadili Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi wa Mwaka 2020 (The Appropriation Bill, 2020) (hatua zote).

Pia, kujadili Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka,2020(TheFinanceBill,2020) ( kusomwa mara ya pili, Kamati ya Bunge zima na kusomwa mara ya tatu] kasha Bunge hilo litapitisha Azimio la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni kuhusu Marekebisho ya Kanuni za Bunge.

Siku hiyo, itahitimishwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutoa hotuba yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!