Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge kuanza, taarifa ya CAG kuchambuliwa
Habari za Siasa

Bunge kuanza, taarifa ya CAG kuchambuliwa

Bunge la Tanzania
Spread the love

VIKAO vya Kamati 14 za Kudumu za Bunge, vinatarajia kuanza tarehe 21 Oktoba 2019 hadi Novemba Mosi mwaka huu. Anaripoti Hamisi Mguta…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 16 Oktoba 2019 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Ofisi ya Bunge.

Taarifa hiyo imeleeza kuwa, miongoni mwa shughuli zitakazofanyika katika vikao hivyo, ni uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu hesabu zilizokaguliwa za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

Pia, Kamati hizo zitafanya uchambuzi wa Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma katika mashirika na taasisi mbalimbali nchini.

Na uchambuzi wa Sheria ndogo zilizowasilishwa wakati wa mkutano mkuu wa kumi na sita wa Bunge.Pamoja na Kupokea na kujadili taarifa ya mapendekezo ya mwongozo wa kutayarisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!