March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bunge, Chadema watifuana

Spread the love

GOGORO kubwa limeibuka kati ya ofisi ya Spika wa Bunge la Jamhuri kwa upande mmoja na familia ya aliyekuwa mbunge wa Buyungu, Mwalimu Kasuku Bilago na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa upande mwingine. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma …  (endelea).

Mgogoro wa sasa umeibuka kufuatia hatua ya ofisi ya Bunge, kuamua kutaka Jumatano wiki hii, kuwa ndiyo siku ya mazishi ya Mwalimu Bilago, kinyume na matakwa ya familia na chama chake.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya familia ya marehemu na uongozi wa Chadema uliongozwa na mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Mbowe, mazishi ya mbunge huyo yatafanyika Alhamisi wiki hii.

Lakini Bunge, huku likijua kuwapo kwa makubaliano hayo, lilitangaza kuwa mazishi ya mwanasiasa huyo yatafanyika Jumatano.

Hadi saa tano na nusu usiku wa Jumatatu, pande hizo mbili zilikuwa hazijaweza kukubaliana juu ya siku rasmi ambayo msiba huo utafanyika.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili, mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema, kinachosababisha kuwapo kwa mvutano huo, ni “Bunge kutotaka kusikiliza wafiwa halisi.”

Mbatia ambaye ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na abmbaye amekuwa akiwaongoza wabunge wa upinzani bungeni anasema, “ni vizuri jambo hili likapatiwa ufumbuzi wa haraka.”

Habari kamili tutawaletea muda si mrefu

error: Content is protected !!