June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunduki za SMG 7 “zaporwa” Tabora

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP), Advera Bulimba

Spread the love

BUNDUKI saba (7) aina ya SMG zinadaiwa kuporwa kutoka katika ghala la kutunzia silaha mkoa wa Tabora. Anaandika Edson Kamukara … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Jeshi la Polisi mkoani Tabora na Makao Makuu wamekwepa kuzithibitisha, watuhumiwa wa sakata hilo ni Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa Tabora ASP Peter Buruna na askari wa kawaida wa wanne.

MwanaHALISIOnline limedokezwa kuwa watuhumiwa hao wamekaa mahabusu ya Polisi zaidi ya wiki mbili sasa na kwamba tayari wameletwa makao makuu jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi wa kina.
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Suzy Kaganda kuthibitisha tukio hilo, alipokea simu na kusema, “nipo safarini nje ya nchi kikazi, naomba atafutwe msaidizi wangu”.

Naye Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP), Advera Bulimba, “alikwepa” akitaka atafutwe kamanda Kaganda. Alipoelezwa kuwa yuko safarini nje ya nchi, msemaji huyo naye alidai yuko nje ya ofisi. 

error: Content is protected !!