March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bundi azua taharuki bungeni, Ndugai atoa neno

Spread the love

NDEGE aina ya bundi amekutwa ndani ya Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma na kuzua taharuki leo asubuhi tarehe 29 Januari 2019. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Baadhi ya wabunge na wageni waliofika bungeni hapo walionekana kumshangaa ndege huyo huku wakibaki na maswali namna alivyoingia kwenye ukimbi huo uliokuwa umefungwa.

Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Job Nduga, Spika wa Bunge aliwatoa hofu wabunge na wageni kuwa, katika mazingira ya kawaida ndege aina ya Bundi kwa wenyeji wa Kabila la Wagogo akitokea mchana hana tatizo isipokuwa Bundi wa usiku.

Hata hivyo, hakuna aliyejua huyo bundi ameingiaje ndani ya ukumbi wa Bunge hasa kutokana na usalama na usafi ndani ya ukumbi huo.

error: Content is protected !!