BAADHI ya wadau wa haki za binadamu nchini Tanzania, wametaka serikali kukunjua makucha yake kwa kuanzisha uchunguzi maalum kwa watumishi wa umma, wanaotuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Miongoni mwa wanaotajwa kuwa wanastahili kuchunguzwa, ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda; aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti na mkuu wa wilaya ya Rorya, mkoani Mara, Simon Ezekiel Odunga.
Mnyeti na Makonda, wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, wakati wakiwa viongozi wa umma, katika kipindi cha utawala wa Hayati Rais John Pombe Magufuli.
Kabla ya kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, Mnyeti ambaye kwa sasa, ni mbunge wa Misungwi, mkoani Mwanza, alikuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.

Makonda, aliondoka kwenye utumishi wa umma, tarehe 15 Julai 2020, baada ya uteuzi wake kufutwa na Hayati Rais Magufuli, kufuatia hatua yake ya kujitosa kwenye mbio za ubunge katika jimbo la Kigamboni.
Kwa nini Makonda, Mnyeti na Onduga wachunguzwe? Kipi wanatuhumiwa kukitenda? Soma Gazeti la Raia Mwema la leo Jumanne, tarehe 8 Juni 2021.
Leave a comment