November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bundesliga kuanza kutimua vumbi leo

Spread the love

BAADA ya kusimama kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19, hatimaye Ligi Kuu ya soka nchini Ujerumani ‘Bundesliga’ imerejea tena leo huku michezo sita ikitarajiwa kuchezwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 18, imerudi leo itachezwa bila uwepo wa mashabiki uwanjani kutokana na katazo la mikusanyiko ya watu katika maeneo ya umma lililotolewa na serikali ya nchi hiyo katika kuendeleza mapambano dhidi ya Corona.

Katika michezo hiyo ya leo Borussia Dortmund itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani “Signal Iduno Park” ambapo itaikalibisha Schalk 04, huku Hoffenheim itaikabili Hertha, Augsburg dhidi ya Wolfsburg, Dusseldorf itawaalika Paderborn, RB Leipzig dhidi ya SC Freiburg na mchezo wa mwisho utakuwa Eintracht Frankfurt dhidi ya Monchengladbach.

Mpaka Ligi hiyo inasimama tayari ilikuwa ishachezwa michezo 25 huku klabu ya Bayern Munich ikiwa kinara kwa baada ya kujikusanyia jumla ya alama 55, huku klabu ya Paderborn ikishika mkia ikiwa na alama 16.

error: Content is protected !!