Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Bumbuli: Sijaridhika na hukumu, nitakata rufaa
Michezo

Bumbuli: Sijaridhika na hukumu, nitakata rufaa

Hassan Bumbuli, Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga
Spread the love

 

MARA baada ya kufungiwa miaka mitatu kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hajaridhishwa na hukumu hiyo na leo hii atawasilisha rufaa yake. Anaripoti kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamati hiyo ilimpa adhabu hiyo Bumbuli mara baada ya kushindwa kulipa kiasi cha Sh. 5,000,000 kama ilivyoainishwa kwenye hukumu yao iliyotolewa tarehe 28 Septemba 2020, mara baada ya kiongozi huyo kukutwa na hatia.

Taarifa ya kamati hiyo ya maadili iliyotolerwa jana tarehe 27 Januari 2021, imeeleza kuwa adhabu ya kumfungia kiongozi huyo kwa kipindi cha miaka mitatu imetolewa chini ya cha 73(8)(a) cha mwongozo wa maadili ya TFF, toleo la 2013.

Akizungumza mara baada ya adhabu hiyo Bumbuli amesema kuwa hukumu hiyo imeshatoka na wameipokea ila kwa upande wake bado hakulizika na maamuzi hayo na atakata rufaa ambayo wataiwasilisha leo.

“Nyundo imeshuka na tumeshaipokea na tutaijadili na uongozi wa yanga tujue tunafanyaje, na kiufupi hatukulizika na hukumu ilivyotoka kama ilivyokuwa ya awali na tutakata rufaa ambayo tutaiwasilisha hii leo,” alisema Bumbuli.

Aidha Bumbuli aliendelea kusema kuwa hata baada ya kumpa adhabu ya mwanzo hukumu haikueleza kuwa anatakiwa alipe hiyo pesa ndani ya muda gani licha ya kamati kumueleza kuwa rufaa ipo wazi.

“Ilipotoka adhabu ya mwanzo mimi niliomba kukataa rufaa na ili niweze kukata rufaa nilitakiwa kufuata taratibu kwa kuwa mara baada ya kunitia hatiani waliambia rufaa ipo wazi na hukumu haikusema nilipe hiyo pesa ndani ya muda gani na baadae tulipokaa na uongozi tukaona bora tulipe.

“Nilienda kwenye kamati Jumamosi na nikaiambia kamati kwamba nilishalipa na niliwapelekea risiti ya Banki TFF kuonesha kwamba kwamba nimeshalipa ila wao hawajanipa hiyo risiti,” aliongea Msemaji huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!