January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bulembo atoa wito kukusanywa michango

Spread the love

BARAZA Kuu la Jumuiya ya Wazazi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) limewatangazia vita walimu wakuu wa shule za sekondari za jumuiya hiyo ambao watabainika kutopeleka michango ya wanafunzi wa shule hizo katika ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya hiyo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo mjini hapa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa, Abdallah Bulembo wakati alipokuwa akifungua kikao cha utendaji kazi cha baraza kuu la jumuiya hiyo.

Bulembo amesema kuwa, wakuu wote wa shule za jumuiya ya chama hicho wanatakiwa kupelekea michango ya sh 100,000 Makao Makuu ambayo hutolewa na wanafunzi wanaojiunga na Kidato cha Kwanza katika shule hizo.

“Michango hiyo imeanishwa kwenye fomu za maelekezo ya kujiunga na shule hizo ambapo tayari wanafunzi hao walitoa fedha hizo lakini bado baadhi ya wakuu wa shule hawajapeleka makao makuu ya chama chetu hivyo nawasisitiza kupeleka haraka fedha hizo.

“Endapo agizo hili halitatekelezwa na wakuu hawa wa shule zetu za jumuiya itabidi waandike barua haraka za kuacha kazi ili tuwaweke pembeni na sheria zichukue mkondo wake,” amesema.

Mwenyekiti huyo aliwataka wakuu hao wa shule kutofanya kazi zao kwa mazoea na badala yake wawe makini katika utendaji kazi wao kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni za kazi zilizowekwa.

“Hivi sasa jumuiya imekuwa ikifanya ukaguzi wa fedha katika shule hizo lakini walimu ambao watabainika kufanya ubadhirifu tutawaondoa shuleni ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani na kwa wale watakaosalimika wataendelea na kazi,” amesema

Hata hivyo amesema kuwa, baadhi ya walimu ambao wamekuwa wakihamishwa shule hukataa endapo hawataki kazi waseme ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Mbali na hilo Bulembo amesema kuwa, walimu wote wa shule hizo kutofanya siasa shuleni kwakuwa zimekuwa zikipunguza ufanisi wa kazi kwa walimu.

error: Content is protected !!