Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bulembo ataka CCM imshughulikie Mpina
Habari za SiasaTangulizi

Bulembo ataka CCM imshughulikie Mpina

Luhaga Mpina, Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Spread the love

 

MWENYEKITI mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo amekiomba chama hicho kumchukulia hatua mbunge wake wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa kutokuwa na nidhamu na viongozi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Bulembo amesema hayo siku moja kupita tangu Mpina amshukie vikali Waziri wa Nishati, January Makamba kwa uamuzi wa kufuta tozo ya Sh.100 ya kila lita ya mafuta.

Makamba alitangaza uamuzi huo tarehe 28 Februari 2022 kwa kupindi cha miezi mitatu Machi hadi Mei ili kupunguza makali ya bei ya mafuta inayotokana na vita ya Urusi na Ukraine.

Katika kupindi hicho, Serikali ingekosa mapato ya Sh.90 bilioni ambazo ni sawa na Sh.30 kila mwezi.

Andallah Bulembo

Hata hivyo, Rais Samia ameagiza kurejeshwa kwa tozo hiyo kwani ni tathimini haikufanyika vyema kutokana na tozo hiyo kuwa tayari imepitishwa kwenye bajeti.

Jana Jumatano tarehe 6 Aprili 2022, Mpina aliwaeleza waandishi wa habari kuwa alichokifanya Waziri Makamba alivunja Katiba, sheria na ni uhujumu uchumi hivyo Takukuru wanapaswa kumchukulia hatua.

Mpina alikwenda mbali na kueleza katika mkutano huu wa Bunge wa bajeti unaoendelea atakwenda kusema mambo magumu yanayohusu nchi ambayo hayaelezwi kama miradi ya Bwawa la Umeme wa Julius Nyerere, kupanda kwa mfumko wa bei bila kuogopa vitisho vya watu au kikundi cha watu.

Kauli hiyo ya Mpina aliyewahi kuwa waziri wa mifupo na uvuvi imemwibua Bulembo ambaye amesema,”Luhaga Mpina amesema ataenda kamati ya bunge kuiomba iunde tume ya kumjadili aliyemwita muhujumu uchumi Waziri Makamba, binafsi nimepata shida kwani nimekaa bungeni. Mpina anawezaje kujadili kauli ya Rais hadharani, kwa kuwa alichosema January kilisemwa na Rais.”

Bulembo amesema,”Kama Waziri Makamba angesema tuongeze Sh.100 kutoka kwenye bei halali tungesema amecheza dili na wauza mafuta ili wapate pesa, lakini amempunguzia Mtanzania ili apate afueni, eti anaonekana muhujumu uchumi.”

January Makamba, Waziri wa Nishati

Mbunge huyo wa zamani wa Kuteuliwa amekwenda mbali na kusema,”Mimi ningemsihi Mzee Abdulrahman Kinana angeanza na Luhaga Mpina, kwa kuwa CCM ina maadili na kila Mbunge wa CCM ana miiko. Ndani ya CCM kuna Caucas yani ukiwa na jambo lako unalipeleka hapo, ukitoka hadharani kama Mpina kuisema serikali ni kukosa maadili.”

Kinana ni Makamu Mwenyekiti wa CCM- Bara ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya maadili ya chama hicho tawala.

Bulembo amesema, Luhaga Mpina huyu alichokifanya ni kumpa shida bosi wetu ambaye ni Rais, lakini tozo imeondolewa sawa, kesho Rais akisema anaongeza bilioni 100 kwa ajili ya kumpunguzia mwananchi mzigo, kuna mtu atachukia? Kwa kuwa walioko bungeni wanatuwakilisha sisi.

“Mimi niliwahi kuomba bungeni kuunda tume dhidi ya Luhaga Mpina akiwa ni Waziri wa Mifugo kwani alivunja mitumbwi ya watu alinyang’anya nyavu, ukienda Morogoro ukamtaja Mpina ni shida amenyang’anya ardhi kubwa za watu, ukitaka kutoa boriti ni lazima uwe mwangalifu,” amesema Bulembo

1 Comment

  • Duh!
    Ni nani anampa shida hakim? Mtoa taarifa au mkaa kimya?
    Naomba Bulembo ukae chini…wewe siyo mbunge halafu Mama alishasema, watu waachwe watoe maoni. Maoni ya Mpina na Mama Samia yapo pamoja…wewe ndiye unayeleta wivu.
    Kama huna hoja ya kumtetea January Makamba, usimuingize Mama eti kachafuliwa. Wewe umetoa maoni gani ya hizo tozo?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!