July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bulaya alia na kikokotoo kipya ataka kirudishwe asilimia 50

Mbunge wa Bunge la Tanzania, Esther Bulaya

Spread the love

 

MBUNGE wa Bunge la Tanzania, Esther Bulaya ameitaka Serikali kuachana na kikokotoo kipya cha mafao kinachompa mstaafu asilimia 33 ya mafao yake na kutaka kirudi cha asilimia 50. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Bulaya ameyasema hayo leo Jumanne tarehe 21 Juni, 2022 akichangia hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 bungeni jijini Dodoma.

Bulaya amesema kwa kikokotoo kipya mtu anayepokea mshahara wa ngazi ya TGTS 1 anayepata mshahara wa Sh1,235,000 kiinua mgongo kitakuwa Sh. 47 milioni kwa kikokotoo cha sasa lakini kwa kikokotoo cha zamani angelipwa Sh95 milioni na kupaki na pensheni ya 500,000 kwa miaka 15 badala ya miaka 12 ya sasa.

“Mmeleta sheria ya kikokotoo cha kuwaminya watumishi, sio sawa tuliambiwa msubiri na wadau mmekutana nao mmeleta asilimia 33 halafu mnajisifia wakati kile cha asilimia 25 mlibadilisha wenyewe,” amesema Bulaya.

Amehoji sasababu ya kutaka kubaki na asilimia 67 ya fedha za watumishi “ambao wanapata mishahara midogo, wanaweza kukaa miaka mitano bila kuongezewa mshahara, mtumishi ambaye hajajenga, mtumishi ambaye hana biashara.”

Bulaya amesema Serikali imepunguza kiasi hicho kwasababu mifuko haina hela ya kuwalipa kwasababu Serikali imeikopa na haijarudisha fedha.

Mbunge huyo alihoji sababu ya bajeti kuu kututenga Bilioni 2 kwaajili ya kulipa mifuko hiyo kama ilivyofanya mwaka unaoishia.

Amesema licha ya wadau kushauri mshahara wa mwisho kutumika kukokotoa mafao yao lakini Serikali imekataa na kusisitiza kutumia mshahara bora wa miaka mitatu ndani ya kipindi cha miaka 10.

Amesema wafanyakazi wamekaa kimya kwasababu ya wawakilishi wao “kubanwa” kwenye vikao, “leo hakuna chama cha wafanya kazi chenye gut ya kutoka na kusema na mimi nawaambia achene kuwasaliti watumishi ndiyo watekelezaji wa mpango”

Ameitaka Serikali kubadilisha kanuni na kwenda kukaa na wadau kuwasikiliza ili kubadilisha kikokotoo hicho.

error: Content is protected !!