July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bulaya akwamisha kesi ya vigogo Chadema

Viongozi wa Chadema wakiwa mahakamani kusikiliza kesi yao ya uchochezi

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na kuumwa kwa mshitakiwa wa tisa kwenye kesi hiyo, Esther Bulaya. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). 

Bulaya, mbunge wa Bunda Mjini, anadaiwa kuwa mgonjwa na amelezwa kwenye hospitali ya Aga Khan na hivyo kushindwa kufika mahakamani.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni mbunge wa Hai na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe; katibu mkuu wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji, Naibu Katibu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika.

Wengine, ni pamoja na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe na mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema taifa (BAWACHA); Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko.

Kesi hiyo, ilikuja mahakamani leo tarehe 28 Machi, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa. Iko mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, aliambia mahakama kuwa kesi hiyo imekuja mahakamani kwa ajili ya usikilizaji ambapo upande wa mashataka umejianda kwa ajili ya ushahidi na tayari mashahidi wawili wako mbele ya mahakama yake.

Hata hivyo, Nchimbi alisema, shauri hilo haliwezi kuendelea kutokana na mshatakiwa Namba tisa kutokuwapo mahakamani.

Kufuatia madai hayo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala, akaieleza mahakama kuwa mshitakiwa huyo ni mgonjwa na mbele ya mahakama yako, yupo mdhamini wake. Akatoa vielelezo kuthibitisha ugonjwa wa Bulaya.

Mdhamini wa Bulaya katika kesi hiyo, ni Ndeshukurwa Tungaraza, diwani wa Chadema katika kata ya Makongo. 

Diwani huyo amedai kuwa hali ya afya ya Bulaya sio mzuri na kwamba ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kushindwa kutembea.

Tungaraza amesema, “mheshimiwa Hakimu, Bulaya yupo mapumzikoni kwa uangalizi wa afya yake kutokana na upasuaji aliofanyiwa tarehe 23 Machi kwenye hospitali ya Aga Khan iliyokuwepo Dar es Salaam alipolazwa tangu 22.

Baada ya kumaliza hayo mdhamini huyo aliwasilisha mahakamani hapo cheti cha Daktari kilichokuwa kikieleza hali ya afya ya Bulaya.

Kibatala aliileza mahakama kuwa pamoja na kutokuwepo kwa mshtakiwa huyo kutokana na hali ya afya yake, lakini ameridhia kuendelea kwa shauri hilo.

Hakimu Simba amesema kuwa uwepo wa mshatakiwa kwenye ksei yake, ni suala la kisheria; ni ridhaa ya mshitakiwa kuruhusu kesi iendelee bila kuwapo mahakamani ili baadaye asije kudai kuwa hajapata nafasi ya kusiliza au kusikilizwa.

Naye Nchimbi amedai kuwa Kifungo cha 199 cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai kinaeleza kuwa ushahidi wowote unaotolewa mahakamani utolewe mbele ya mshtakiwa.

Ameendelea kueleza pia kifungu la 197(20) la mwenendo wa makosa ya jinai kimeweka wazi kuwa Mahakama inaweza kupokea ushahidi endapo mshtakiwa asipokuwepo mahakamani awe na tatizo la kiafya na ameridhia kutolewa kwa ushahidi huo, awe na Mwakilishi (wakili).

Baada ya hapo wakili Kibatala amemuomba Hakimu Simba washauriane na upande wa mashtaka ili kuona namna ya kuwasilisha kwa ridhaa ya mshitakiwa.

Hakimu Simba, aliekeza kuwa ridhaa ya mshitakiwa Bulaya, iwasilishwe mahakamani kwa barua au kwa njia ya kiapo.

Baada ya kunong’onezana na upande wa mashtaka, wakili Kibatala akaomba shauri lisogezwe mbele ili kupatikane ridhaa ya maandishi ya Bulaya.

Hakimu Simba ameahilisha shauri na kusikilizwa mfululizo tarehe 16 na 17 Aprili mwaka huu.

error: Content is protected !!