May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Buku 7000 tu, kuiona Simba na Yanga

Spread the love

 

KLABU ya Simba imetangaza viingilio vya mchezo wao dhidi ya Yanga utakaochezwa Jumamosi ya tarehe 8 Mei, 2021, ambapo kiingilio cha chini kitwakuwa Sh. 7,000 kwa mzunguko. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo, mbali na kiingilio cha mzunguko, viingilio vingine vya mchezo huo vitakuwa Sh. 15,000 kwa  VIP C, VIP B Sh. 20,000 na VIP itakuwa Sh. 30,000.

Timu hizo zinaingia kwenye mchezo huo, huku zikiwa zinafukuzana kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ambapo Simba inashika nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 61, baada ya kucheza michezo 25 na Yanga ipo nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 wakicheza michezo 27.

Tayari waamuzi wa mchezo huo wameshatangazwa, ambapo mwamuzi wa kati atakuwa, Emmanuel Mwandembwa kutoka Arusha, huku waamuzi wasaidizi Frank Komba na Hamdani  Saidi kutoka Mtwara, na mwamuzi wa akiba, Ramadhani Kayombo.

error: Content is protected !!