August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Buhari: Sitaki kuombwa radhi

Spread the love
 MUHAMMADU Buhari, Rais wa Nigeria amekataa kuombwa radhi na David Cameroon, Waziri Mkuu wa Uingereza aliyelitaja taifa lake (Nigeria) kuwa ni miongoni mwa mataifa yaliyo na ufisadi mkubwa, anaandika Wolfram Mwalongo.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripoti kwamba, Cameroon alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Malkia Elizabeth wakati wa hafla ya kupambana na ufisadi London, Uingereza.
Hata hivyo, Buhari amesema kwamba, angependa kurudishiwa mali yote iliyoibiwa kutoka Nigeria na kuingiza kisha kuzuiwa kwenye Benki za Uingereza.
Hata hivyo, Buhari amekiri kwamba Nigeria ni miongoni mwa mataifa yaliyo kwenye orodha ya juu katika ufisadi ambapo linashika namba 136 katika nchi 167 kulingana na taarifa iliyotolewa na Shirika la Transparency International ya mwaka 2015.
error: Content is protected !!