December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Buguruni, Ilala, Kinondoni, Mwenge kushuhudia mwili wa Dk. Mengi

Spread the love

MWILI wa Dk. Reginald Abraham Mengi, aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni zilizo chini ya IPP Group, unatarajiwa kuletwa leo saa 8:30 mchana. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Usalama umeimarishwa katika sehemu mbalimbali, hususan maeneo mwili huo utapitishwa baada ya kufikishwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalim Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kutoka Dubai, Falme za Kiarabu.

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amezungumza na wananchi na kueleza barabara ambayo mwili huo utapitishwa pale utapoanza safari kutoka JNIA saa 9:45.

Barabara hizo ni Vingunguti, Buguruni, Ilala, Kigogo, Magomeni (Kanisa  Katoliki), Kinondoni, Morocco, Makumbusho, Bamaga, ITV, Mwenge kuelekea Hospitali ya Lugalo.

“Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa likiwamo Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, tumejipanga kuimarisha usalama katika maeneo yote ambako mwili wa mpendwa wetu, Dk. Mengi utapita,” amesema Makonda na kuongeza;

“Alifafanua kuwa, siku ya kwanza ni leo ambayo mwili utaletwa, siku ya Jumanne ambayo utaagwa katika viwanja vya Karimjee na siku ya Jumatano utakaposafirishwa kuelekea Machame wilayani Hai, Kilimanjaro kwa maziko siku ya Alhamisi.”

error: Content is protected !!