Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko BRELA yakutana na wadau kupitia Kanuni za Wamiliki Manufaa wa Kampuni
Habari Mchanganyiko

BRELA yakutana na wadau kupitia Kanuni za Wamiliki Manufaa wa Kampuni

Spread the love

 

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imekutana na Vyombo vya Uchunguzi kwaajili ya kupitia Kanuni za Wamiliki Manufaa wa Kampuni zinazomilikiwa na wabia kwa lengo la kuziboresha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akifungua warsha ya siku moja katika ukumbi wa Zimamoto, Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara, Meinrad Rweyemamu, amesema lengo la warsha hiyo ni kupeana elimu ya kiutendaji kwa wadau na watumiaji wa taarifa za wamiliki manufaa.

“BRELA tumekuwa tukishirikiana na wadau kwenye shughuli zetu mbalimbali za kiutendaji ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho mbalimbali ya kisheria na kimfumo lengo ni kuhakikisha tunatoa huduma bora kwenu na kwa umma kwa ujumla,” amefafanua Rweyemamu.

Rweyemamu amesema kuwa Kampuni zina umuhimu mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi, “hata hivyo uzoefu umeonyesha kwamba kampuni nyingine zinatumika vibaya katika kufanya vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na utakatishaji wa fedha haramu, kufadhili vitendo vya ugaidi, vitendo vya rushwa na hata ukwepaji wa kodi.”

Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara, Meinrad Rweyemamu

Kutokana na hali hiyo amesema Benki ya Dunia na taasisi nyingine za Kimataifa zinazojihusisha na masuala ya kusaidia biashara zimejitolea kuleta mabadiliko kwa kuanzisha dhana ya Wamiliki Manufaa ( Beneficial Ownership concept) ambayo imeungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.

Ameongeza kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo zipo chini ya Eastern and Southern Anti-Money Laundering Group (ESAMLAG), ambapo lengo lake ni kuhakikisha kuwa mapendekezo 40 yanafanyiwa kazi.

“Moja kati ya mapendekezo hayo ni kuhakikisha nchi inaanzisha daftari la Wamiliki Manufaa wa Kampuni na kuhakikisha vyombo vya uchunguzi vinapata taarifa za wamiliki manufaa kwa wakati,” amesema.

Aidha ameongeza kuwa Sheria ya Kampuni Sura 212 ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria ya Fedha, 2020 kwa kuleta dhana ya Umiliki Manufaa wa Kampuni.

Marekebisho hayo yalienda sambamba na utungwaji wa Kanuni za Wamiliki Manufaa za mwaka 2021 ambazo zinatumika katika kusimamia zoezi la ukusanyaji, uwasilishaji na utoaji wa taarifa za wamiliki manufaa wa kampuni.

Amesema pia Wakala imeona ni vyema kuandaa warsha ya kuwashirikisha wadau mbalimbali kujadili na kukusanya maoni yao ili kuboresha rasimu ya Kanuni zilizoandaliwa na kuweka utaratibu madhubuti utakaowezesha upatikanaji wa taarifa za wamiliki manufaa wa majina ya biashara pamoja na utoaji wa taarifa hizo kwa vyombo vya upelelezi vilivyoainishwa kwenye Sheria pale zinapohitajika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!