Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko BREAKING NEWS-Saba wafariki ajali ya gari, mkokoteni Dodoma
Habari MchanganyikoTangulizi

BREAKING NEWS-Saba wafariki ajali ya gari, mkokoteni Dodoma

Spread the love

 

WATU saba wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Landcruiser yenye namba za usajili STL 9534 mali ya Idara ya maji mkoa wa Katavi, kugonga kwa nyuma mkokoteni uliokuwa unavutwa na ng’ombe katika Kijiji cha Lugala- Kata ya Manzase wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ajali hiyo imetokea leo tarehe 3 Julai, 2022 saa 11 alfajiri wakati gari hiyo ikitokea Dodoma kuelekea Mtera kugonga mkokoteni huo uliokuwa ukikokotwa na ng’ombe wawili huku ukiwa umepakia abiria 12.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea ajali hiyo na kubainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa gari hiyo.

Amesema mbali na watu hao saba, pia ng’ombe wawili waliokuwa wakikokota mkokoteni huo, nao pia wamefariki kutokana na ajali hiyo.

Amesema gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Paschal Sitta mkazi wa Katavi, alikuwa akiendesha gari hiyo kwa mwendokasi ambao ulimsababisha kushindwa kung’amua iwepo wa mkokoteni huo mbele yake kwa haraka.

“Kwa sababu muda huo wa alfajiri hilo eneo huwa linakuwa na ukungu kidogo, sasa kwa kuwa dereva alikuwa speed kwa uelekeo sawasawa na huo mkokoteni kama wanaelekea Iringa, alipoukaribia mkokoteni huo na ukizingatia huaukuwa na alama zozote nyuma, basi akaugonga, ukapinduka, watu saba wakafariki papo hapo, na ng’ombe wawili,” amesema.

Amesema majeruhi watano wa ajali hiyo wamewahishwa katika hospitali ya General mkoani Dodoma kwa ajili ya matibabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

error: Content is protected !!