Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Breaking news! Azam FC yamtimua Kocha Mkuu
Michezo

Breaking news! Azam FC yamtimua Kocha Mkuu

Spread the love

 

BODI ya Klabu ya Azam FC imesitisha mkataba na Denis Lavagne, kama kocha mkuu, kuanzia leo tarehe 22 Oktoba, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Imeelezwa kuwa uamuzi huo ni kwa maslahi mapana ya klabu na mustakabali wa mradi wake wa maendeleo ya kiufundi.

Denis Jean Lavagne, raia wa Ufaransa, alijiunga na Azam FC 7 Septemba, mwaka huu akisaini mkataba wa mwaka mmoja uliomtaka aifikishe klabu kwenye angalau hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika.

Kwa bahati mbaya mahitaji hayo ya kimkataba hayakufikiwa hivyo bodi ikafikia uamuzi huu.

Kwa sasa timu itakuwa chini Kalimangonga Sam Daniel Ongala na Agrey Moris hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Bodi inamshukuru Lavagne kwa jitihada zake za kuisaidia klabu yetu na weledi mkubwa aliouonesha alipokuwa nasi.

Aidha inamtakia kila la heri huko aendako.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!