Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Branch kufikisha mikopo ya haraka kwa mamilioni ya Watanzania
Habari Mchanganyiko

Branch kufikisha mikopo ya haraka kwa mamilioni ya Watanzania

Spread the love

BRANCH, kampuni inayoongoza duniani kwa utoaji mikopo kwa watu binafsi kwa njia ya simu za mikononi, imeelezea nia yake thabiti ya kuwafikishia huduma za kifedha za gharama nafuu mamilioni ya Wanzania popote pale walipo.

Tangu kuanzishwa kwake hapa nchini mwaka 2015, Branch tayari imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 73 na kuwafikia zaidi ya watu milioni moja na laki tano walipo sehemu mbali mbali.

Mikopo ainayotolewa na Branch kupitia App yao inaanzia kiasi cha shilingi 5,000 hadi shilingi 1,000,000.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari leo tarehe 4 Julai, 2022 Msimamizi wa huduma kwa wateja kwa Tanzania, Reuben Wanyamawi amesema Branch imejipanga vyema kuwafikishia huduma za mikopo  Watanzania popote pale walipo na muda wowote hivyo kuwezesha kutatua changamoto zao zinazohitaji fedha.

“Branch inayofuraha kuwahudumia Watanzania na mkakati wetu ni kuwafikia Watanzania wengi zaidi popote pale walipo na muda wowote. Ni jambo la kuvutia kuona kuwa  idadi ya watu wanaotumia huduma zetu imekuwa ikiongezeka kila kukicha,” alisema

Reuben ameongeza, “Tunaamini kuwa kila mtu popote pale lipo anahitaji na anastahili huduma za kifedha. Kuongezeka kwa matumizi ya simu janja kunaongeza fursa kwa watu wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha,”

Msimamizi wa Huduma kwa wateja wa Kampuni ya Kutoa mikopo kwa njia ya simu za mkononi kupitia App ya Branch Reuben Wanyamawi (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha Ya Pamoja na wanahabari jijini Dar es Dalaam, muda mfupi baada ya kuelezea mpango wa kampuni hiyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

Kwa mujibu wa msimizi huyo wa huduma kwa wateja, inachukua dakika chache tu kwa mtu kuomba mkopo na kuupata kupitia App ya Branch. “Ukishathibitishwa, inachukua dakika chache tu kupata mkopo wako. Tunatumia taarifa zilizopo kwenye simu za wateja kufanya maamuzi ya kutoa mikopo. Kama ombi lako halijakubaliwa, usijali. Wakati mwingine huchukua mara kadhaa kuomba ndiyo mteja apate mkopo,” lmesema

Katika kuhakisha wateja wanafurahia huduma zao alisema, Branch ina utaratibu wa rufaa ambapo kama mteja akimshawishi mteja mwingine kuchukua mkopo na akaulipa kwa wakati, mteja huyo atapata zawadi ya shilingi 7,000 na mteja mpya atapata zawadi ya shilingi 7,000 pia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!