January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Boti ya Tanzania yanaswa na unga Scotland

Boti ya Hamal Zanzibar ikiwa chini ya ulinzi na meli ya ulinzi ya Scotland baada ya kukutwa na dawa za kulevya

Spread the love

BOTI yenye usajili wa Tanzania, imekamatwa kwenye Bahari ya Kaskazini na baada ya kupekuliwa katika bandari ya Arberdeen huko Scotland, imekutwa na shehena ya dawa zakulevya. Anaandika Benedict Kimbache … (endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, boti hiyo inayoitwa Hamal, yenye urefu wa mita 32 na uwezo wa kubeba tani 422, ilizuiwa Alhamisi na vyombo viwili vya ulinzi vinavyofanya doria ikiwa umbali wa maili 100 kutoka usawa wa bahari mashariki mwa mji wa Arberden.

Kwa mujibu wa mtandao unaoonyesha vilipo vyombo vya baharini, katikati ya Februari,  boti hiyo ilikuwa Uturuki na wiki mbili zilizopita ilianza safari kutoka visiwa vya Tenerife huko Hispania na ilipokamatwa ilikuwa inaelekea Hamburg, mji wa pili kwa ukubwa wa Ujerumani ikitazamiwa kufika usiku wa Ijumaa iliyopita.

Boti hiyo imekutwa na watu 9 wenye umri kati ya miaka 26 na 63 na wameshtakiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya wakitarajiwa kupelekwa mahakamani. Hata hivyo watu hao utaifa wao haukuweza kupatikana mara moja.

John McGowan wa mamlaka inayoshughulikia uhalifu kitengo cha ulinzi wa mipaka (NCA-BPC), amesema boti hiyo imekamatwa na kiwango kikubwa cha dawa za kulevya na kukamatwa kwake kumewezekana kutokana na ushirikiano wa taasisi za ulinzi za Uingereza na ushiriiano wa kimataifa.

“Kiasi kamili cha dawa hizo bado hakijafahamika na upekuaji bado unaendelea kwa ushirikiano wa NCA na Jeshi la Polisi ya Scotland,” amesema.

error: Content is protected !!