Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa BoT yatuhumiwa mbele ya Rais Magufuli
Habari za Siasa

BoT yatuhumiwa mbele ya Rais Magufuli

Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
Spread the love

AMANI Kibondei, Mfanyabiashara wa Ubadilishaji Fedha za Kigeni katika Jiji la Dar es Salaam, ameishtaki Benki Kuu ya Taifa (BoT) kwa Rais John Magufuli, akidai kwamba, baadhi ya maofisa wake wamekuwa wakivuruga biashara hiyo. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara takribani 1,000 uliofanyika leo tarehe 7 Juni 2019, Ikulu jijini Dar es Salaam, Kibondei amedai kwamba, baadhi ya maofisa wa BoT wamekuwa na desturi ya kuvamia maduka ya ubadilishaji fedha za kigeni na kuchukua fedha hizo.

Kibondei ameeleza kuwa, maofisa hao walivamia katika maduka yake matatu kati ya matano anayomiliki jijini Dar es Salaam, na kubeba fedha zote zilizomo kwenye maduka hayo.

“Mwezi wa pili  mwaka huu BoT walikuja wakavamia na kuchukua fedha zote , kwa kutumia fomu ambazo huwa wanakuja kutukagulia kila mwaka, baada ya wiki moja au siku kumi na nne wanatuletea ripoti kwamba, kuna makosa haya utajirekebishaje ama unalipishwa faini.

“Kilichofanyika sasa ni kwamba, fedha zote wamechukua hawakubakisha hata shilingi mia wakaondoka nazo, nilikuwa na matano yakabaki mawili, hayajakaguliwa. Nimekuta maofisa wamevamia wakachukua kila kitu.”

Mfanyabiashara huyo amelalamika kuwa, alipouliza maofisa hao sababu za kuchukua fedha hizo pasipo kueleza makosa yake, alijibiwa kwamba hatua hiyo ni utekelezwaji wa maagizo kutoka juu.

“Watu wananicheka kwamba, wenzio wamefunga wee unaendelea, unajiamini sana? nikawaambia mimi sina makosa watakagua wanachokitaka, nimetoka BoT nimefika ofisini kwangu, nimekuta wamevamia na kuchukua kila kitu.

“Nikawaambia mi nitaishi vipi? wakasema hata Sh. 50 si tutaitafuta kwa tochi, nikawaeleza nina majukumu nitaishi vipi, wakasema hayo ni maagizo,” amesema Kibondei.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!