July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

BOT yatetea sarafu ya 500

Spread the love

BENKI Kuu ya Tanzania BOT imesema sarafu ya Tsh 500 itaendelea kutumika nchini mpaka pale ambapo noti ya fedha hiyo zikapoisha na kutoonekana mitaani. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea)

Hayo yamsemwa wakati wa mazungumzo na waaandishi wa habari kuhusu Majukumu ya mfumo mpya wa huduma za kibenki wa TIS utakaotumika kufanya malipo muhimu yakiwemo malipo ya kodi.

Mkurugenzi wa huduma za kibenki kutoka BOT, Marcian Kobello amesema kupotea kwa sarafu hiyo katika maeneo mbalimbali nchini kunatokana na Benki mbalimbli kuwaa na tabia ya kuchukua fedha kutoka benki Kuu ambazo zenye thamani kubwa zikiwemo noti za elfu kumi na elfu tano na kuacha fedha zenye dhamani ndogo kama 500 hasa sarafu.

Kobello amesema hadi sasa Benki kuu ya Tanzania imesimamisha kutengeneza mia tano za noti kutokana na mzunguko wake kuwa mkubwa, hali inayopelekea fedha hiyo kuchakaa haraka.

Amesema amezitaka Benki kuwa na tabia ya kuchukua fedha zenye thamani ndogondogo ikiwemo sarafu ya Tsh 500 iliyoanzishwa mwaka Oktoba mwaa jana ili kuongeza mzunguko wa fedha hizo na kupunguza uchakavu wa fedha za noti.

Akizungumzia mfumo mpya wa TIS, Mkurugenzi wa Mfumo huo, Bernard Dady amesema ni mfumo ambao unawezesha huduma za kibenki kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa bei nafuu na kwa uharaka zaidi.

Kobello amesema kwa sasa mfumo huo utawezesha benki zote kufanya kazi hadi usiku kwa ajili ya kuboresha huduma na kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na mfumo huo.

error: Content is protected !!