January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

BoT yakarabati Makumbusho ya Nyerere

Nyumba ya Makumbusho ya Mwalimu Nyerere

Spread the love

BENKI Kuu wa Tanzania (BoT) imetoa Sh. 50 milioni kwa ajili ya kukarabati wa Nyumba ya Makumbusho ya Mwalimu, Julius Nyerere iliyopo kijijini kwake Mwitongo, Butiama mkoani Mara. Anaandika Moses Mseti … (endelea).

Kutolewa kwa fedha hizo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa mwaka jana na BoT, ambapo hundi hiyo ilikabidhiwa kwa Mkuu wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere na Kaimu Gavana wa BoT, Juma Reli.

Akikabidhi hundi hiyo, Kaimu Gavana wa benki hiyo, amesema waliahidi kutoa fedha hizo mwaka jana, baada ya kutembelea makumbusho ya Mwalimu Nyerere.

“Mwaka jana tulitembelea Makumbusho ya Mwalimu Nyerere yaliyopo Butiama Mkoa wa Mara, wenzetu wa makumbusho wakatuomba msaada wa kufanya matengenezo ya nyumba hiyo ambayo ni sehemu ya historia kwa vizazi vijavyo,” amesema Reli.

Naye, mkuu wa makumbusho hayo, Emmanuel Kiondo, amesema wanawashukuru BoT, kwani nyumba hiyo ni muhimu kwa historia ya taifa hili.

Amesema nyumba hiyo itakuwa ni mfano kwa baadhi ya vijana hapa nchini kuacha kutegemea nyumba za wazazi wao pindi wanapoingia kwenye ndoa.

“Unajua nyumba hiyo ni nyumba ambayo Mwalimu Nyerere alianzia maisha, kwa mila na desturi za kwao kijana alikuwa haruhusiwi kuoa kama hana nyumba, hivyo Mwalimu aliamua kujenga na baadaye alimuoa mama Maria Nyerere na kuishi naye hapo kwa zaidi ya miaka 30 akiwa Rais,” amesema Kiondo.

error: Content is protected !!