August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

BoT yafafanua kuhusu dhamana kukuza uchumi

Spread the love

BENKI kuu ya Tanzania (BOT) imewataka wananchi kununua dhamana za serikali ili kuchangia katika kukuza uchumi wa taifa, anaandika Aisha Amran.

Haya yamesemwa leo na Alexander Ngwinamila Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa BOT jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema dhamana za serikali hutolewa kama uthibitisho wa serikali kukopa kwa wananchi(Exchange for money borrowed from public)na baadae kulipa fedha hizo kwa riba kulingana na kiwango kilichowekezwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za uwekezaji kwenye dhamana za serikali.

Alieleza taratibu na faida za kuwekeza kwenye dhamana za serikali ni salama kwani serikali haitarajiwi kukiuka mategemeo ya wadai wake wakati wa malipo.

Pia alizitaja faida nyingine kuwa amana za serikali zinahamishika hivyo mwekezaji anaweza kuziuza kabla ya muda wake wa kuiva na zinaweza kutumika kama dhamana kwa ajili ya mkopo.

Amesema dhamana za serikali zimekuwa zikiuzwa kwenye soko la awali kwa njia ya mnada wenye ushindani kwa kila wiki.

Amefafanua wakati mwingine kwenye soko la upili dhamana za muda mrefu huuzwa na kununuliwa wakati wowote ambapo mnada wa dhamana za serikali unaendana na kalenda inayotengenezwa na serikali kila mwaka.

Amefafanua watu wanaoruhusiwa kushiriki kwenye mnada huo ni watanzania pamoja na wananchi wote wa Afrika mashariki wanahaki ya kushiriki knunua dhamana ya serikali.

Amesema viwango vya ushiriki katika ununuzi wa dhamana hizo unaanzia shilingi laki 5,00000 kwa dhamana za muda mfupi na 1,000,000 milioni za muda mrefu au hati fungani.

Benki kuu ya Tanzania kama wakala wa serikali imepewa wajibu wa kuuza dhamana za serikali kwa muda mfupi na muda mrefu.

error: Content is protected !!