Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Bosi Takukuru aomba kukiri makosa uhujumu uchumi
Habari Mchanganyiko

Bosi Takukuru aomba kukiri makosa uhujumu uchumi

Spread the love

MKURUGENZI wa zamani wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor, ameiomba Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuharakisha mchakato kujibu ombi lake la kukiri makosa yanayomkabili katika kesi uhujumu uchumi inayomkabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Leo Jumatatu tarehe 12 Oktoba 2020, Eliya Mwigira, wakili wa Kulthum, mbele ya Hakimu Mfawidhi Godfrey Isaya ameiomba Ofisi ya DPP kuharakisha mchakato wa kujibu maombi ya mshtakiwa ya kukiri makosa katika kesi hiyo kwa kuwa tayari kashakamilisha taratibu zote za maombi.

Awali, Wakili Mwandamizi wa Serikali Wankyo Simon ameieleza Mahakama hiyo shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kuipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa.

Shauri hilo limeahirishwa mpaka tarehe 26 Oktoba 2020.

Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP)

Katika kesi hiyo, mshtakiwa Kuluthumu anakabiliwa na mashitaka manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh.1.477 bilioni.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshtakiwa alighushi barua ya ofa ya Agosti 13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo huku akijua kuwa sio kweli.

Katika shtaka la pili, inadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017 maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshitakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh.5.2 milioni kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru kama malipo ya kiwanja kilichopo Kijiji cha Ukuni Bagamoyo.

Pia, inadaiwa kati ya tarehe hizo, Mansoor alijipatia Sh.3 milioni kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Mshtakiwa huyo pia alijipatia Sh.5 milioni kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo hilo.

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi wa TAKUKURU

Katika shtaka la tano, inadaiwa Mansoor alijipatia Sh.7 milioni kutoka kwa Ekwabi Majungu ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.

Pia, anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathminu alijipatia Sh milioni saba kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.

Indaiwa kuwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Rose Shingela kwa ajili ya malipo hayo.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko maeneo ya Upanga, mshitakiwa alijipatia Sh.1.477 bilioni wakati akijua fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!