RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amemteuwa Ghalib Said Mohammed kuwa Mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Tunisia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Ghalib ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya GSM ambao ni wafadhili wa kuu wa klabu ya Yanga ataongoza kamati hiyo ambayo ina wajumbe 13.
Viongozi wengine wa kamati wa kamati hiyo ni Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye ni makamu mwenyekiti, huku katibu wa kamati hiyo ni Mhandisi Hersi Said ambaye ni mjumbe wa mashindano klabu ya Yanga.

Wajumbe walioteuliwa kwenye kamati hiyo ni Abdallah bin kleb, Haji Manara, Jerry Muro, Patrick Kahemele, Zacharia Hanspope, Beatrice Singano, Christina Manyenye, Said Nassor.
Wengine ni Anitha Rwehumbiza, Farid Nahdi, Feisal Abri, Farough Baghozal, Nandi Mwinyimbella na Phelomen Ntahijala.
Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Africa, AFCON dhidi ya Tunisia utakaopigwa 13 Novemba, 2020.
Leave a comment