BOSI wa kikundi cha mafia maarufu kama Cosa Nostra anayesakwa zaidi nchini Italia, Matteo Messina Denaro amekamatwa huko Sicily baada ya kutoroka kwa miaka 30. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa vyombo vya kimataifa … (endelea).
Matteo Messina Denaro alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2002 kwa makosa ya mauaji mengi.
Matteo ambaye pia alijulikana kama Diabolik alizaliwa tarehe 26 Aprili 1962 anadhaniwa kuwa mrithi wa Bernardo Provenzano ambaye alikamatwa Aprili 11 mwaka 2006.
Inasemekana kuwa Matteo alijifunza kutumia bastola akiwa na miaka 14 na alifanya mauaji yake ya kwanza kati ya mengi akiwa na miaka 18 tu.
Inakadiriwa kuwa Matteo ameua takribani watu 50 na alijipatia umaarufu baada ya kumuua bosi wa mafia ya Alcamo, Vincenzo Milazzo.
Baba yake Francesco Messina Denaro maarufu Don Ciccio alikuwa mkuu wa kamisheni ya mafia ya Trapan na alikuwa mwanzilishi wa kikundi cha ulinzi cha kulinda ardhi ya familia.
Leave a comment