Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Biashara Bosi utalii atoa ujumbe wa mikopo nafuu ya NMB
BiasharaHabari

Bosi utalii atoa ujumbe wa mikopo nafuu ya NMB

Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Dk. Francis Michael amewataka wadau wa utalii jijini Arusha kutumia fursa ya mikopo nafuu ya Benki ya NMB katika kuwekeza kwenye sekta ya utalii ili kuvutia wageni nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza katika kongamano la utalii (Tourism Networking) lililofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki, Dk. Michael alisema NMB imekuwa chachu katika kuhakikisha inawapa mikopo wadau wa sekta ya utalii katika kuimarisha mazingira ya vivutio nchini.

“Tunaomba mfanye jitihada za kuijenga sekta ya utalii kwani serikali imeshaweka mazingira ya kuitangaza kupitia filamu ya Royal Tour ambapo hadi sasa kuna baadhi ya hoteli zimeshajaa wageni.”

“Hivyo ni kitu cha kujivunia kwetu na nyie kama wadau ni vyema mkatumia fursa hiyo katika kuweka mazingira sawa,” alisema Dk. Michael.

Dk. Michael alisema wadau wa utalii wanapaswa kutumia vema fursa waliyopewa na Benki ya NMB kwa sababu ni taasisi muhimu ya kifedha inayoshiriki kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na ubunifu nchini.

Alisema, fedha watakazotengewa kwa ajili ya mikopo wazitumie vema ili wazirudishe na wengine wapate fursa ya kuzipata kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza idadi ya watalii nchini kwa maendeleo ya sekta zote.

Alisisitiza wadau wa utalii wahakikishe wanatumia vema fursa waliyopewa na Benki ya NMB kikamilifu ili kuimarisha usalama kwa watalii wanapokua nchini, ikiwemo kutumia vituo vya polisi vinavyohudumia watalii lengo likiwa ni kuongeza idadi ya watalii na kuwafanya wapate sababu za kurejea tena baada ya kurudi kwao.

“Hiki kinachofanywa na NMB ni kitu kikubwa sana, kifikirieni na mkitumie vizuri kwa sababu fursa kama hizi haziji mara mbili. Wafurahisheni watalii ili wakienda kwao wakawalete watu wengine na wao warejee tena na tena,” alisema Dk. Michael.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi alisema benki hiyo wanaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya utalii nchini.

“Tunafanya kila namna kuhakikisha tunaunga mkono maono ya Rais Samia. Utalii ni sekta muhimu katika uchumi wa nchi yetu, hapa katikati kulitokea mtikisiko mkubwa wa UVIKO-19 ambao ulikimbiza watalii, lakini sasa hakuna sababu ya kushindwa kutumia fursa ya vivutio tulivyo navyo kuwarudisha waje nchini, hasa baada ya Rais Samia kutufungulia njia kupitia filamu ya Royal Tour,” alisema Mponzi.

Aidha, Mponzi alisisitiza kwa miaka ya hivi karibuni NMB imeanza kutoa huduma ya mikopo katika sekta ya utalii lengo ni kuimarisha katika kutoa huduma kwa wageni wanaofika nchini kutalii na kuona vivutio vilivyopo nchi nzima.

“Bado tunaendelea kutoa katika sekta ya utalii kwa lengo la kufanya vizuri zaidi na sasa tumejipanga kuwahudumia wageni wote wanaofika nchini, ili wakirudi kwao wapate sababu ya kurejea tena nchini,” alisema Mponzi.

Benki ya NMB wiki kadhaa zilizopita walikutana na wadau wa utalii visiwani Zanzibar ambapo waliwaahidi kuwapa mikopo mbalimbali kuanzia maboti na miradi mingine itakayohamasisha watalii kutembelea visiwa hivyi vyenye utajiri wa historia na mambo ya kiasili.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Habari

Tanzania yaungana na nchi 180 kushiriki maonesho ya utalii Ujerumani

Spread the love  TANZANIA imeungana na mataifa 180 duniani kushiriki maonesho makubwa...

error: Content is protected !!