Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Bosi Takukuru atangaza mabadiliko ya viongozi
Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi Takukuru atangaza mabadiliko ya viongozi

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imefanya mabadiliko ya uongozi, sambamba na kuanzisha huduma inayotembea (Mobile PCCB), kwa ajili ya kuboresha utendaji wake ili kuendana na mazingira ya sasa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya mabadiliko hayo, imetolewa leo Jumatano tarehe 13 Januari 2021, na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, wakati anatoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa wanahabari, jijini Dar es Salaam.

Mbungo amesema, mabadiliko hayo yanahusu watendaji katika safu ya wakurugenzi, wachunguzi pamoja na wakuu wa Takukuru wa mikoa.

“Mabadiliko haya, yamezingatia utendaji wa taasisi na mazingira ya sasa yalivyo. Nadhani wenzetu watatusaidia vizuri kupambana na rushwa kwenye maeneo waliyopangiwa,” amesema  Mbungo.

Mkuu huyo wa Takukuru, ametaja mabadiliko hayo kuwa ni, nafasi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi ambayo itashikiliwa na Isidory Kyando, aliyekuwa Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara, kabla ya uteuzi huo.

“Nafasi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi itashikiliwa na Kyando. Aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo, atahudumu katika nafasi nyingine katika makao makuu,” amesema  Mbungo.

Katika mabadiliko hayo, Neema Mwakalyelye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (Tehama), huku Leornada Ngaiza akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ndani. Wakati Malimi Mifuko akishika nafasi ya Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki.

Aliyekuwa Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Rukwa, Hamza Mwenda amehamishiwa kuwa Mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Ruvuma.

Yustina Chagaka, aliyekuwa Mkuu wa Takukuru mkoani Ruvuma, amehamishiwa Mkoa wa Rukwa.

Aliyekuwa Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Njombe, Domina Mkama, amehamishwa kuwa mkuu wa taasisi hiyo mkoani Iringa.

Frida Wikesi, aliyekuwa Afisa Mchunguzi Mkuu makao makuu ya taasisi hiyo,  amekuwa Mkuu wa Takukuru Kilimanjaro.

Huku aliyekuwa Afisa Mchunguzi Mkuu Makao Makuu ya Takukuru, Kassim Ephrem amepangiwa kuwa Mkuu wa taasisi hiyo mkoani Njombe.

Aliyekuwa Mkuu wa Takukuru mkoani Mara, Alex Kuhanda, amehamishiwa makao makuu ya taasisi hiyo.

Hassan Mossi, aliyekuwa Mchunguzi Mkuu Ofisi ya Takukuru mkoani Mwanza, amehamishwa kuwa Mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Mara.

Wakati aliyekuwa Mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Lindi, Stephen Chami, amehamishiwa makao makuu.

Aliyekuwa Afisa Uchunguzi Makao Makuu ya Takukuru, Abnery Mganga, amepangiwa kuwa Mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Lindi.

Huku aliyekuwa Mchunguzi Mkuu katika Makao Makuu ya taasisi hiyo, Frank Mkilanya amepangiwa kuwa Mkuu wa Takukuru Mwanza.

Emmanuel Stenga, aliyekuwa Mkuu wa Takukuru mkoani Mwanza, amehamishiwa makao makuu ya taasisi hiyo. Wakati James Ruge aliyekuwa Mchunguzi Mkuu Makao Makuu, amekuwa Mkuu wa Takukuru mkoani Arusha.

Kuhusu utaratibu wa huduma ya Takukuru inayotembea, Mbungo amesema taasisi hiyo imetenga siku moja maalumu kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa kila mkoa.

“Kuanzia Januari 2021 tumeanzisha utaratibu wa Mobile PCCB, kwa kutenga siku moja kila mwezi ambapo kila ofisi ya Takukuru mkoa na wilaya itawafuata wananchi huko walipo, kwa lengo la kusikiliza pamoja na kutatua kero zao,” amesema Mbungo.

Mbungo ametoa ratiba ya utoaji wa huduma hiyo kwa mwezi Januari mwaka huu. Hii hapa chini …

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!