May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bosi Nida akalia kuti kavu, Waziri Simbachawene asema…

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene, amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Anold Kihaule, akae kando kama kazi ya kuongoza mamlaka hiyo imemshinda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Simbachawene ametoa agizo hilo jana Jumatatu, tarehe 19 Julai 2021, katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.

Simbachawene ametoa malekezo hayo baada ya kubaini changamoto katika utendaji wa NIDA, zilizopelekea mamlaka hiyo kushindwa kuzalisha vitambulisho vya Taifa vya kutosha.

“Tangu nimeingia kwenye uwaziri, kelele zote nilizopiga kuhusu vitambulisho zimezalisha milioni mbili. Siwezi kukubali ninachomwambia mkurugenzi kama kazi imemshinda awaachie watu wengine.”

“Ni mteule wa Rais lakini kama kazi imemshinda atafute kazi nyingine,” alisema Simbachawene.

Kwa mujibu wa Simbachawene, NIDA imetengeneza vitambulisho milioni mbili, idadi ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya Watanzania wasiopungua milioni 50.

error: Content is protected !!