Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bosi NEC amvaa Lissu ‘Watanzania hawataki bla bla’
Habari za SiasaTangulizi

Bosi NEC amvaa Lissu ‘Watanzania hawataki bla bla’

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera
Spread the love

DAKTARI Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, ameonesha kukasirishwa na kile alichoita wanasiasa kudanganya na kutoa tuhuma badala ya kunadi sera za elimu, barabara, afya na umeme. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Ametoa kauli hiyo jana Jumapili tarehe 27 Septemba 2020 wakati akimtuhumu Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kusema uongo dhidi ya Dk. John Magufuli, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema, Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho-Bara, alisema Dk. Magufuli aliitisha kikao cha wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo yote nchini, jijini Dodoma kwa ajili ya kupanga mikakati ya kuhujumu uchaguzi.

          Soma zaidi:- 

Amemteka kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya tume hiyo kujieleza tarehe 29 Septemba 2020.

“Tunawataka wagombea kujali muda wa kampeni, ratiba za kampeni, kuepuka matusi kwa sababu unatumia muda mwingi kutangaza matusi badala ya sera.”

“Unatumia muda mwingi kutangaza tuhuma badala ya sera, unatumia muda mwingi kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi badala ya kutangaza sera sera,” amesema Mahera mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha

“Watanzania sasa hivi wanataka afya iliyoimarika, Watanzania wanataka barabara nzuri, Watanzania wanataka miradi ya umeme, Watanzania wanataka elimu iliyobora, Watanzania hawataki blabla.”

“Watanzania wanataka sasa viongozi watakaolinda madini yao siyo viongozi watakaochukua madini yao na kupeleka kwa wegeni,” amesema

“Tumemwandikia barua Lissu kumtaka kufika kwenye kamati ya maadili tarehe 29 Septemba 2020,” amesema na kuongeza “…tumemuita Lissu ili aje kutoa maelezo na ushahidi kwa kile alichokisema.

Pia amesema, zipo taarifa kwenye mitandao ya kijamii zilizodai, yeye (Mahera) alifanya kikao na Rais Magufuli na wasimamizi wa majimbo yote ya uchaguzi.

Hata hivyo, amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na badala yake zililenga kutoa taharuki kwa Watanzania na kutengeneza mazingira iaminike kuwa uchaguzi hautakuwa huru na haki.

“Wanataka kutoa picha ili iaminike kwamba uchaguzi huu hautakuwa huru na haki, na kwamba hata wakishindwa kihalali watataka Watanzania wawaunge mkono kuvuruga amani ya nchi, kwa kuwa wana ajenda zao binafsi,” alisema.

Alisema, tangu Septemba 25 na 26 mwaka huu, amekuwa akiendelea na ziara yake ya kikazi kukagua na kuratibu maandalizi ya uchaguzi katika majimbo ya mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Aliongeza kuwa katika ziara hiyo, amekutana na wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo ya kazi, hivyo tuhuma za Lissu zina lengo baya kwa nchi na kuichafua tume.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!