September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bosi KADCO afariki dunia

Mhandisi Christopher Mukoma, Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO)

Spread the love

MHANDISI Christopher Mukoma, Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO), amefariki dunia leo Ijumaa tarehe 8 Mei 2020, kutokana na tatizo la shinikizo la damu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo na Julius Nyamkama, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakati akizungumza na MwanaHALISI ONLINE kwa simu.

Nyamkama amesema Mhandisi Mukoma alifariki dunia akiwa nyumbani kwake mkoani Arusha, baada ya kusumbuliwa na shinikizo la damu.

Amesema marehemu alianza kusumbuliwa na tatizo hilo siku mbili zilizopita.

“Ni kweli Mhandisi Mukoma amefariki dunia leo akiwa nyumbani kwake Arusha. Alikuwa anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu na alianza kuumwa siku mbili zilizopita,” amesema Nyamkama.

error: Content is protected !!