August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Bosi’ Jamii Forums mfupa mgumu kwa serikali

Maxence Melo, Mwanzilishi wa Mtandao wa Jamiiforum

Spread the love

UPANDE wa Jamhuri umeshindwa kukamilisha upelelezi wa kesi ya kumiliki mtandao bila kusajiliwa hapa nchini  inayomkabili Maxence Melo Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Jamii Media inayomiliki mtandao wa Jamii Forums, anandika Faki Sosi.

Mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, mwendesha mashitaka wa serikali Mohammedi Salimu amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na hivyo ameomba  kesi hiyo ihairishwe mpaka tarehe nyengine.

Hata hivyo, Hakimu Simba ameitaka serikali kukamilisha upepelezi haraka katika kesi hiyo Na. 456 yenye shtaka moja tu ambapo Melo anadaiwa kuwa, kati ya tarehe Mosi Aprili na 13 Desemba 2016, akiwa Mkurugenzi wa  Kampuni ya Jamii media inayoendesha mtandao wa Jamii Forums alikataa kutoa kwa Jeshi la Polisi taarifa za kiuchunguzi zilizochapishwa kwenye mtandao huo.

Wakati huo huo mtuhuhumiwa Melo anakabiliwa na kesi nyengine Na.  457 mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa, ambapo pia mwendesha mashitaka wa serikali Mohamedi Salumu amedai kuwa upepelezi haujakamilika pia.

Kesi zote mbili zimeahirishwa na zitatajwa tena tarehe 26 Januari 2017.

error: Content is protected !!