May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bosi Bandari mikononi mwa Takukuru

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (PTA), Mhandisi Deusidedit Kakoko

Spread the love

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanania, inamshikilia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA), Desdedit Kakoko, kwa uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Ni baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kumsimamisha kazi Jumapili ya tarehe 28 Machi 2021, kutokana na ubadhirifu wa fedha zaidi ya Sh.3.9 bilioni.

Rais Samia, alitoa maagizo hayo, mara baada ya kupokea ripoti mbili za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nay a Takukuru zote za mwaka 2019/20, Ikulu ya Chamwoni, mkoani Dodoma.

Bandari Dar es Salaam Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema, wanamshikilia Kakoko na wanaendelea kumhoji juu ya tuhuma mbalimbali dhidi yake.

Akitoa agizo la kusimamishwa kwa Kakoko, Rais Samia alisema “imani yangu ni kwamba, kama kuna ubadhirifu ndani ya shirika na kwa ripoti ile uliyonipa jioni, kuna uibadhirifu Sh. 3.9 Bil. karibu Sh. 4 Bil. Waziri Mkuu(Kassim Majaliwa) alivyofanya ukaguzi walisimamishwa wa chini, naomba nitoe agizo la kumsimamisha mkurugenzi mkuu wa bandari halafu uchunguzi uendelee.”

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!