July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bosco Ntaganda akutwa na hatia

Bosco Ntaganda

Spread the love

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), imemtia hatiani kwa makosa ya uhalifu wa kivita na binadamu Bosco Ntaganda,  kiongozi wa zamani wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Majaji wa ICC wamemkuta na hatia Ntaganda kwa makosa 18 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, uliotokea katika Mji wa Mashariki wa Ituri mwaka 2002 na 2003.

Robert Fremr, Jaji wa ICC amesema, Ntaganda anatuhumiwa kutoa amri zenye lengo la kuuwa na kutesa raia wasio na hatia, alipokuwa kiongozi wa waasi.

Makosa mengine yaliyotajwa na waendesha mashtaka hao ni pamoja na kuhusishwa na vitendo vya ubakaji na utumwa wa ngono, kumuuwa kasisi wa kikatoliki pamoja na kuwasajili watoto kwenye jeshi wakiwemo wasichana.

Vile vile, Ntaganda anatuhumiwa kuongoza operesheni ya waasi wa Union of Congolese Patriots (UCP).

error: Content is protected !!