August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bondia Mashali kuzikwa leo

Thomas Mashali enzi za uhai wake

Spread the love

THOMAS Mashali, mmoja kati ya mabondia mashuhuri nchini Tanzania, atazikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Mashali ambaye ana rekodi ya kipekee kwenye mchezo huo, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana Kimara, jijini Dar es Salaam.

Mashali ameaga dunia akiwa na rekodi mwanana kwenye mchezo huo baada ya kucheza mapambano 25 na kushinda 19 ambapo alipoteza matano, sare moja na KO 4.

Miongoni mwa mambo ambayo Mashali aliyalalamikia kwenye kongamano lililofanyika mwaka huu ni pamoja na tabia ya mapromota kunyanyasa mabondia kwenye mapambano.

Bondia huyo amekuwa akisafiri kwenye nchi mbalimbali kutokana na kazi yake ambapo mwaka jana alikwenda Nairobi, Kenya kufanya mazoezi akiwa na mabondia wengine wawili kabla ya kusafiri kwenda Ulaya.

Mashali aliyezaliwa tarehe 9 Septemba, 1989. Alijiunga na ndondi za kulipwa mwaka 2009. Pambano lake la kwanza mwaka huo lilifanyika tarehe 11 Novemba dhidi ya Hamadu Mwalimu katika Ukumbi wa Manzese Texas, Dar es Salaam ambalo alishinda kwa KO.

Pambano la pili la Mashali lilifanyika tarehe 4 Aprili 2010 dhidi ya Super Middle ambapo mwisho wa mchezo alikwenda sare na mpinzani wake.

Kabla ya kufariki, pambano lake mwa mwisho lilifanyika tarehe 12 Septemba mwaka huu Bagamoyo, Pwani dhidi ya Shabani Kaoneka. Kwenye pambano hilo Mashali alishinda kwa pointi.

error: Content is protected !!