July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bonanza la Shimmuta kufanyika Oktoba

Spread the love

BONANZA la Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), ambalo lilipangwa kufanyika Septemba 26 mwaka huu limesogezwa mbele na kufanyika Oktoba 10 mwaka huu. anaandika Faki Sosi … (endelea).

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa SHIMMUTA, Award Safari, na kusema kuwa, sababu za kusogezwa mbele kwa bonanza hilo ni kutokana na siku hiyo imegongana na mechi kubwa ya ligi kuu ya watani wa jadi ambao ni Simba na Yanga.

Amesema kuwa hadi kutolewa taarifa hii kwenye vyombo vya habari timu 12 za taasisi, mashirika na makampuni mbalimbali yamethibitisha kushiriki katika bonaza hilo kwa tarehe hiyo iliyotajwa.

Safari amezitaja timu hizo za kutoka katika baadhi ya makampuni ya Dar es Salaam kuwa ni, TTCL, CBE, MOI, TPA, TANESCO, MUHAS, TPDC, IFM, TBS,na UDSM.

Na timu nyengine kutoka mikoani ni Chuo cha Kilimo cha Morogoro (SUA) na Chuo Cha Ufundi Cha Arusha.

Michezo itaanza saa 12 asubuhi na kuisha saa 12 jioni ambako kutakuwa na mechi za Mpira wa Miguu,Netiboli , kuvutana kwa kamba, kukimbia ukiwa na kijiko chenye ndimu mdomoni, kukimbia ukiwa ndani ya gunia   kutunga uzi kwenye sindano huku ukikimbia,kula “apple”likiwa linaning’inia na kukuna nazi kwa wanaume ambapo timu zote watafanya mazoezi ya viungo pamoja.

error: Content is protected !!