Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Bonanza la NMB vuta nikuvute lafana Zanzibar
Michezo

Bonanza la NMB vuta nikuvute lafana Zanzibar

Spread the love

BENKI ya NMB ikiwa inaendeea kusherehekea safari yake ya mafanikio ya miaka 25, iliandaa bonanza la Michezo waliloliita Vuta Nikuvute visiwani Zanzibar. Kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Benki ya NMB, kilitawazwa mabingwa wa tamasha la michezo la kudumisha ushirikiano baina ya benki hiyo na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung, Visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).


Shujaa wa timu ya NMB inayonolewa na nyota wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mohammed Hussein ‘Mmachinga,’ alikuwa ni mshambuliaji Simon Zubeir, aliyetikisa nyavu mara tatu ‘hat trick,’ mabao yote akiyafunga kipindi cha pili, baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa sare tasa, huku kila upande ukionesha kiwango bora. 


Bonanza hilo lilitanguliwa na matembezi ya hisani yaliyoshirikisha wafanyakazi wa NMB, Wajumbe wa Baraza la Mawaziri Zanzibar wachezaji wa timu za michezo yote na kikundi cha mbio za taratibu ‘jogging’ cha Island Exercise Club, huku washiriki wote wakiongozwa na Mgeni Rasmi, Zubeir Ali Maulid, ambaye ni Spika wa Baraza la Mawaziri Zanzibar pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Ruth Zaipuna.

Bonanza hili lilijumuisha michezo ya mpira wa miguu, mpira wa kikapu, netiboli, kuvuta kamba, mbio fupi za mita 100, mbio za magunia na kufukuza kuku, ambako ukiondoa soka, NMB pia ilitwaa ubingwa kuvuta kamba (wanawake), mbio za mita 100 (wanaume).


Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi, timu zake zilitwaa ubingwa katika mchezo ya kikapu (wanaume) walikoshinda pointi 53-42, netiboli (wanawake) magoli 36-21, mbio za magunia wanaume, kuvuta kamba (wanaume) na mbio za mita 100 (wanawake).

Akizungumza viwanjani hapo, Bi. Ruth, alimuahidi Spika wa Baraza la Wawakilishi kuwa, NMB itaendelea kutoa mchango wa kustawisha sekta ya michezo visiwani Zanzibar, kwani anamini michezo ni afya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!