April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bombadier ya Tanzania yakamatwa Canada, Prof. Kabudi achimba mkwara

Moja ya ndege za Bombadier inayomilikiwa na Tanzania

Spread the love

NDEGE aina ya Bomberdier Q 400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania, inashikiliwa nchini Canada, kwa amri ya mahakama. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hayo amesema Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, leo tarehe 23 Novemba 2019, jijini Dodoma.

Prof. Kabudi ameeleza kuwa, aliyehusika na ukwamishaji huo, ni Mkulima Hermanus Steyn, aliyewahi zuia ndege nyingine ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), nchini Afrika Kusini, mwezi Septemba mwaka huu. 

“Ndege ambayo ilikuwa ifike Tanzania, imekwama nchini Canada, kesi iko mahakamani na aliyefungua ni yule ambaye aliyeikamata ndege yetu Afrika Kusini, tukamshinda kwenye kesi. Alikata rufaa tena tukamshinda, sasa amekimbilia Canada, amekamata ndege yetu,” amesema Prof. Kabudi.

Aidha, Prof. Kabudi ameeleza kushangazwa na ndege hiyo kukwama nchini Canada, huku akieleza kwamba, ndege zilizonunuliwa nchini Marekani zilifika nchini salama, lakini zilizonunuliwa nchini humo, zinakamatwa.

“Jambo la kusikitisha ndege kutoka Marekani mbili hazikukwama, lakini kila ndege zikitoka Canada zinakwamishwa. Tunashangaa hawa matapeli wanajuaje hadi ndege zinakamtwa?” amehoji Prof. Kabudi.

Kufuatia changamoto hiyo, Prof. Kabudi amesema amemuita Balozi wa Tanzania nchini Canada, kuzungumza kuhusu suala hilo.

Na kwamba, amempa ujumbe ya kuwa, Tanzania haifurahishwi na vitendo vya ndege zake,  kukamatwa nchini humo.

Wakati huo huo, Prof. Kabudi amemshauri Rais John Magufuli, kama inawezekana serikali yake iache kununua ndege nchini Canada.

“Nafikiri Mheshimiwa Rais kukushauri, kama Canada inaruhusu vitu kama hivi, sio peke yao wanaotengeneza ndege, hatukufanya makosa kununua ndege Canada,” amesema Prof. Kabudi.

Aidha, Prof. Kabudi amesema serikali imetuma wanasheria nchini Canada, kwa ajili ya kushughulikia suala hilo.

“Sasa naelewa unalosema (Rais Magufuli) kila unapo ongeza juhudi za kuleta maendeleo, wako wanaokesha kukwamisha. Hao mabeberu wa nje kwa kutumiwa na watu wachache wa ndani,” amesema Prof. Kabudi.

Ndege hiyo aina ya Bomberdier Q400 inakuwa ndege ya pili kuwahi kushikiliwa nchini Canada.

error: Content is protected !!