April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bombadier iliyokamatwa Canada, kuwasili nchini

Moja ya ndege za Bombadier inayomilikiwa na Tanzania

Spread the love

NDEGE iliyoshikiliwa nchini Canada kutokana na amri ya mahakama kufuatia kesi ya madai iliyofunguliwa na Hermanus Steyn, inataraji kuwasili Tanzania wakati wowote. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 28 Novemba 2019 na Injinia Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Kamwelwe ameeleza kuwa, mazungumzo kuhusu suala hilo yamekamilika, na kuwa, ndege hiyo aina ya Bombadier Q 400, itawasili wakati wowote, ingawa hakutaja siku.

Aidha, Kamwelwe amewataka Watanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho juhudi za kuikomboa ndege hiyo zikiendelea.

Ndege hiyo mali ya serikali kwa ajili ya matumizi ya Kampuni ya Ndege ya Taifa (ATCL) imeshikiliwa nchini Canada, baada ya Steyn kufungua kesi katika mahakama ya nchi hiyo, akidai fidia ya mali zake zilizotaifishwa na serikali ya Tanzania mwaka 1980.

error: Content is protected !!