Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Bodi ya Wakurugenzi Dawasa yazinduliwa, yapewa kazi
Habari Mchanganyiko

Bodi ya Wakurugenzi Dawasa yazinduliwa, yapewa kazi

Spread the love

 

WAZIRI wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa), kuisimamia ipasavyo mamlaka hiyo ili itekeleze ipasavyo miradi mbalimbali ukiwemo wa Rufiji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, ameiagiza Dawasa chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Mhandisi Cyprian Luhemeja ianze kufikiria kuanzisha kampuni ili kupanua zaidi wigo wa utoaji wa huduma.

Aweso ameyasema hayo leo Ijumaa, tarehe 17 Septemba 2021, makao makuu ya Dawasa, Mwananyamala, Dar es Salaam wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Dawasa inayoongozwa na Mwenyekiti, Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange.

“Nimshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na nataka kusema, mimi Jumaa Aweso na watendaji wangu wa wizara, hatutakuwa kikwazo cha wana Dar es Salaam na Watanzania kupata maji na wala hatutamuangusha,” amesema Aweso

Amesema, bodi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu, wameisimamia vyema menejimenti ya Dawasa na kuhakikisha inasogeza huduma kwa wananchi na kuanzisha miradi mipya na kuwa mamlaka ya mfano nchini humo.

Moja ya kazi ambayo Waziri Aweso ameipata bodi hiyo ni kusimamia mradi wa kutoa maji mto Rufiji ukamilike kwa wakati.

Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema, mchakato umekwisha kuanza wa mradi huo ambao ni maagizo ya Rais Samia.

Alisema, mahitaji ya maji ifikapo mwaka 2027 itakuwa zaidi ya bilioni moja hivyo mradi huo ni muhimu.

“Mradi wa Rufiji utakamilika na malengo yetu ukamilike kabla ya mwaka 2025 ili uzinduliwe na mheshimiwa Rais Samia,” amesema

Katika maagizo yake kwa bodi, Waziri Aweso ameitaka kutembelea miradi na si kuwa bodi ya vikao na kusoma makaratasi huku akidokeza, chini ya mwenyekiti Mwamungange hakuna shaka kila kitu kitakwenda sawa.

“Wizara ya maji yote ipo Dawasa. Mko vizuri sana. Ukizaa mtoto akawa anafanya vizuri, jukumu kubwa kama mzazi ni kumwombea dua.”

“Niwaombe sana Dawasa kuwa na ulimi mzuri kwa wale mnaowahudumia ili kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri. Mkiwa na ulimi mbaya mambo hayatakwenda,” amesema

Aidha amehoji, iwapo shughuli ya kuwafikishia huduma itakamilika, Dawasa itafanya kazi gani? Sasa “kama maeneo yote yatapata maji, mkimaliza mtafanya kazi gani? Sasa fikirieni kuanzisha kampuni.”

Pia, ameahidi kutoa fedha kugharamikia mradi wa Kigamboni ili ukamilike.

Kwa upande wake, Mwenyeki wa Bodi, Jenerali Mwamunyange ambaye anaendelea kwa kipindi cha miaka mitatu mingine amesema, kila akilala, kuamka anaota ndoto njema juu ya Dawasa.

“Naota miradi mingi inazinduliwa. Mara naota mradi wa Kidunda, mara naota mradi wa Rufiji umezinduliwa,” amesema Jenerali Mwamunganye na kuwafanya wafanyakazi waliokuwepo kushangilia

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amewashkuru wajumbe wa bodi hiyo kwa kwa kukubali “uteuzi huu, sehemu kubwa ya majukumu yenu ni kwenda kujitolea.”

“Tunawaomba muendeleze pale mlipoishia. Lakini tunawashukuru na kuwapongeza Dawasa kwa kuwa wabunifu. Kila mara mnafanya ubunifu mzuri unaoonesha mna watumishi wazuri na tunatarajia Dawasa ya kesho haitakuwa kama ya leo,” amesema

“Wito wangu kwa bodi ni kuhakikisha inatatua changamoto za upatikanaji wa maji maeneo ya pembezeno. Itakuwa ni fahari kuona upatikanaji wa maji maeneo yote,” ameongeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!