June 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bodi ya wadhamini CUF ya Seif yakwaa ‘kisiki’ kortini

Maalim Seif Sharrif Hamad. Picha ndogo Prof. Ibrahim Lipumba

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya bodi ya wadhamini inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, anaandika Faki Sosi.

Maombi hayo yalikuwa yanaiomba mahakama kupokea maombi ya kumshtaki Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwa kosa la kumpatia ruzuku Professa Ibrahimu Lipumba badala ya kuituma kwenye akaunti ya chama.

Hata hivyo, serikali ilipinga maombi hayo yaliyowasilishwa mahakamani hapo na bodi ya chama hicho.
Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Wilfred Ndyansobera wa Mahakama Kuu huku akisema kifungu kilichotumika kuwasilisha maombi hayo siyo sahihi na kwamba anayaondoa mahakamani hapo.

Jaji Ndyensobera amesema kuwa amekubalina na hoja mbili za upande wa Maalimi Seif ikiwamo ya kutaka kufungua kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 19 (13).

Aidha, amekubaliana na hoja ya bodi ya wadhamini iliyopingwa ambapo amesema kuwa masuala hayo yanahitaji ushahidi.

Jaji amesema kuwa waombaji wanaweza kukata rufaa au kufungua upya shauri hilo.
Hata hivyo, CUF ya Maalim Seif ameahidi kufungua tena kesi hiyo kwa kuzingatia vifungu vilivyoelezwa ili kuhakikisha haki inapatikana.

error: Content is protected !!