December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bodaboda wapumzishwa kuingia mjini, ving’ora, ‘spotlight’ marufuku

Waendesha pikipiki (Bodaboda) wakiwa maeneo ya mjini katika shughuli zao za kawaida

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku usafiri wa pikipiki ‘Bodaboda’ kuingia maeneo ya mjini kuanzia tarehe 6 hadi 18 Agosti 2019. Anaripoti Regina Mkonde …(endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tareje 5 Agosti 2019, Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema, polisi wamepiga marufuku hiyo kutokana na ukaidi wa waendesha bodaboda ikiwemo kutozingatia ama kukiuka sheria za usalama barabara.

Kamanda Mambosasa amesema, marufuku hiyo itatekelezwa hadi mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC), unaoendelea jijini humo, utakapomalizika.

“Jeshi la Polisi limepiga marufuku bodaboda kuingia ‘city center,’ kipindi chote cha ugeni huu hatutawaruhusu. Wamekuwa watu hawaelekezeki kirahisi, wanapenda kupita mwendo kasi, wanataka kuingilia misafara ya viongozi, hawavai helment,” amesema Kamanda Mambosasa na kuongeza;

“Nataka kusema, wavumilie katika kipindi hiki. Kuanzia kesho sitegemei mtu akienda tofauti, akienda tofauti tutazungumza naye sentro.”

Wakati huo huo Kamanda Mambosasa amesema, Jeshi la Polisi limepiga marufuku wamiliki wa magari kutumia vifaa vinavyozua taharuki, ikiwemo ving’ora na taa za ‘Spot light’.

“Ving’ora, spotlight hairuhusiwi kwa watu binafsi. Isipokuwa kwa magari ya serikali na yale ya watu binafsi yenye vibali vya kubebea wagonjwa. Ni marufuku ya kudumu taa zote za vimulimuli.”

“Sasa hivi utakuta bajaji imefunga spotlight, unaweza kufikiri kuna msafara kuja kushtuka unakuta sisimizi tu wanapita barabarani.

“Marufuku ya wote walioweka ving’ora, kimsingi na kisheria huwekwa katika magari maalum ambulance nk na si kwa starehe ya mtu. Msako mkali unaanza kuanzia kesho. Watakamatwa magari hayataachiwa vituo mpaka waje na mafundi wao”.

Aidha, Kamanda Mambosasa amewaonya wahalifu akisema kwamba mtu yeyote atakayejaribu kuchafua taswira ya nchi, atakiona.

“Si wakati wa mtu kujaribu kufanya uhalifu ndani ya jiji. Yeyote atakayetaka kufanya chochote kuharibu taswira ya nchi atakiona. Tunataka Tanzania iwe ni mahali salama. Wananchi wote tuwakaribishe wageni lakini tujiepushe matengo ya uhalifu. Yasiyokuwa wstaarabu'” amesema Kamanda Mambosasa.

error: Content is protected !!