August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bodaboda walalamika Kibaha

Spread the love

MADEREVA wa bodaboda katika mji mdogo wa Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani wamelalamikia baadhi ya polisi kwa kupokea faini bila kutoa stakabadhi, anaandika Hamisi Mguta.

Makosa hayo ni pamoja na kutovaa kofia za kujikinga na ajari (element) na kupakia abiria zaidi ya mmoja.

Mmoja wa madereva wa kituo cha mabasi Mlandizi aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Kondo, ameuambia mtandao huu kuwa, mara nyingi polisi wa mji huo wamekua na utaratibu wa kupokea pesa bila kutoa stakabadhi.

“Kwa namna hii kuna wasiwasi wakafanya makosa ya bodaboda kuwa kigezo cha kuwanufaisha wao binafsi, ukiomba risiti unaambiwa pesa unayolipia si bei husika ya faini,” amesema.

Athanus Kitwana, dereva wa bodaboda amesema, mazoea hayo yanakandamiza haki za wanyonge kwakua maisha ya madereva wa bodaboda ni ya hali ya chini hivyo utaratibu wa utoaji lisiti unapaswa kutekelezwa.

Naye Hassan, dereva aliyedai kukamatwa kwa kosa la kutovaa kofia ya kujikinga na ajari wiki iliyopita amesema, baadhi ya polisi jamii wamekua na tabia ya kutumia vyeo vyao kupokea fedha bila kutoa risiti.

Amesema wiki iliyopita alinyimwa lisiti na polisi aliyejulikana kwa jina moja la Boke ambaye haikufahamika mapema cheo chake. Baada ya kutaka kukomboa pikipiki yake na kujibiwa kuwa faini hiyo aliyolipa ni kama kusaidiwa.

“Nilipotakiwa kufika katika kituo kidogo cha Mlandizi kwenda kuchukua pikipiki yangu iliyokua imekamatwa nilitakiwa kulipa Shilingi 60,000 kama faini, nilipomaliza malipo nikadai risiti lakini askari alinijibu hawezi kunipa lisiti kwakua ni pesa ya kunisaidia wakati awali tulielewana nilipe faini na sio anisaidie,” amesema.

error: Content is protected !!